Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:56

Guterres apongeza uchaguzi wa Kenya


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Katibu Mkuu  wa Umoja  Antonio Guterres Jumanne  alizungumza na rais mteule wa Kenya William Ruto kwa njia ya simu, msemaji wa Umoja huo Stephanie Dujarric  amesema.

Dujarric aliongezea kwamba kiongozi huyo wa UN pia atajaribu kuongea na mgombea urais Odinga mshindani wake wa karibu kwenye uchaguzi uliopita Raila Odinda, na hilo litategemea upatikanaji wake. Guterres alielezea kufurahishwa kwake na namna Kenya ilivyoendesha uchaguzi wake, akitumai kwamba mchakato utamalizika haraka iwezekanavyo kwa kufuata katiba iliyopo na muundo wa kisheria.

Wakati huo huo kundi la waangalizi wa uchaguzi huo limesema Jumanne kwamba hesabu yao inaonyesha kwamba Ruto alikuwa mshindi kwenye uchaguzi huo licha ya Odinga kupinga matokeo hayo baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Wafula Chebuti kumtangaza Ruto kuwa mshindi.

Kundi hilo lenye waangalizi kutoka mashirika 15 ya kiraia na kidini lilifanya hesabu yake sambamba na ile ya IEBC na kufikia uamuzi kwamba Ruto alikuwa mbele ya Raila. Kundi hilo la ELOG limesema kwamba Ruto alipata asilimia 50.7 ya kura zilizopigwa wakati Odinda akimfuata kwa karibu kwa asilimia 48.7 kama alivyotangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Kundi hilo limesema hayo mjini Nairobi mbele ya wanahabari kupitia mwenyekiti wake Anne Ireri.

XS
SM
MD
LG