Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:18

Seneta Coons akutana na viongozi wa kisiasa Kenya

Rais Uhuru Kenyatta akizungumza kwa njia ya video na viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki.
Rais Uhuru Kenyatta akizungumza kwa njia ya video na viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Seneta wa Marekani Chris Coons amekutana na rais mteule wa Kenya William Ruto aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita pamoja na mpinzani wake mkuu Raila Odinga ambaye anapinga matokeo hayo.

Walijadiliana kuhusu ushirikiano wa kimkakati kati ya Marekani na Kenya, kuhamasisha amani na usalama katika eneo na njia za kuimarisha uchumi kati ya nchi hizo mbili.

Seneta Coons pia amekutana na Raila Odinga kujadiliana kuhusu ushirikiano wa thamini za kidemokrasia, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa katika ukurasa wa Twitter wa ubalozi wa Marekani.

Hakukuwa na taarifa yoyote iliyosema kwamba uchaguzi ulizungumziwa. Mapema seneta Coons alikutana na rais Uhuru Kenyatta ambapo walifanya majadiliano.

Seneta Coons ambaye anaongoza ujumbe wa Maseneta wa Marekani na wabunge amempongeza rais Kenyatta kwa kuhakikisha amani na uthabiti vimepatikana wakati wa uchaguzi, “tulifurahishwa na amani ambayo Kenya imeendelea kuwa nayo katika kipindi hiki, “ alisema seneta Coons.

Kwa upande wake rais Kenyatta alisema Kenya itaendelea kuwa imara na kusimamia utawala bora ili kuhakikisha nchi inakuwa katika nafasi ya mfano wa demokrasia katika bara kwa kuhakikisha amani kwenye kipindi hiki cha mpito. “ hamu yangu kubwa ni kuona amani inaendelea kuwepo na tunaweza kuonyesha mfano katika bara la Afrika na dunia”, alisema Rais Uhuru Kenyatta.

XS
SM
MD
LG