Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:09

Rais mteule Ruto asema matarajio ya umma yalikuwa makubwa


Rais mteule wa Kenya William Ruto akihutubia mkutano wa waandishi wa habari katika makazi yake rasmi yaliyoko wilaya ya Karen, Nairobi, Kenya, Aug. 17, 2022.
Rais mteule wa Kenya William Ruto akihutubia mkutano wa waandishi wa habari katika makazi yake rasmi yaliyoko wilaya ya Karen, Nairobi, Kenya, Aug. 17, 2022.

Rais mteule wa Kenya William Ruto amesema matarajio ya umma yalikuwa makubwa na hakukuwa na muda wa kupoteza, ameyasema hayo Jumatano baada ya kukutana na maafisa wa uchaguzi kutoka kwenye muungano wake.

Ingawa mpinzani wake Raila Odinga amesema atatoa changamoto ya matokeo ya kura zilizopigwa August 9, Ruto amesema anasonga mbele kuunda utawala wake.

Amesema hakuna eneo lolote nchini humo litakaloachwa, bila kujali itikadi za kisiasa au kikabila.

Rais mteule wa Kenya ameeleza haya: “ Huduma za umma zitakuwa za kitaalamu na ninatarajia kuwa huduma za umma zitakuwa kwa Wakenya wote, kwa usawa, bila upendeleo wowote kwa kabila, kwa jamii au upendeleo wowote katika msimamo wa kisiasa.”

Ameapa kukabiliana na ukabila wa kisiasa kwa kuwatenga watumishi wa umma kutoka kazi za kisiasa na ameahidi kuhamasisha utamaduni wa kisasa ambako kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu kila kitu kwa njia anayotaka na hakuna mtu atakayewaathiri.

Wiiliam Ruto , Rais mteule wa Kenya aliongeza kusema: “Nataka kuwaambia watu wa Kenya, tunapata tena nchi yetu ya kidemokrasia na kila mtu anaweza kuzungumza na mtu yeyote kuhusu lolote, kwa njia yoyote wanayotaka na hakuna mtu atakayewaathiri.”

Wakati huo huo Waziri wa Baraza la Elimu Profesa George Mgoha Jumatano amesema shule zipo tayari kufunguliwa Alhamisi.

Amesema hadi sasa hakuna tishio lolote la usalama nchini ambalo linaweza kuzuia wanafunzi kurejea shule.

XS
SM
MD
LG