Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:00

Uchaguzi Kenya: Maafisa wa kutuliza ghasia wapelekwa kituo cha kitaifa cha kuhakiki kura


Kenya Election
Kenya Election

Maafisa wa ziada wa polisi wa kutuliza ghasia walipelekwa katika kituo cha kitaifa cha kuhakiki kura za uchaguzi wa rais nchini Kenya, baada ya vurugu kuibuka ndani ya ukumbi wa Bomas of Kenya Jumapili alfajiri.

Katika prukushani hizo, mmoja wa wawakilishi wa vyama tanzu akichukua kipaza sauti na kulalamika kwamba uhalifu ulikuwa ukitendeka ndani ya kituo hicho.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, mtafaruku huo ulidhihirisha hali ya hasira na mvutano mkubwa ndani ya ukumbi huo wa kitaifa wa kuhesabu kura wakati nchi hiyo ikisubiri matokeo rasmi ya uchaguzi wa Jumanne iliyopita.

Hayo yamejiri siku chache tangu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya itangaze kuongeza ulinzi hasa kwenye eneo la kuhesabia kura baada ya ugomvi wa mara ya kwanza kutokea uliohusisha mawakala wa Azimio la Umoja wanaomsimamia Raila Odinga kuwashutumu mawakala wa Kenya Kwanza wanaomsimamia William Ruto, kuingilia mfumo wa kuhesabu kura.

Katika kinyang'anyiro cha urais, matokeo kufikia sasa yanaonyesha ushindani mkali kati ya kiongozi wa upinzani anayeegemea mrengo wa kushoto Raila Odinga na mfanyabiashara tajiriri na naibu Rais William Ruto.

Lakini mkanganyiko juu ya kujumlisha kura na vyombo vya habari na kasi ndogo ya tume ya uchaguzi, IEBC, vimezua wasiwasi nchini Kenya, ambalo ni taifa tajiri na tulivu la Afrika Mashariki lakini ambalo lina historia ya ghasia kufuatia chaguzi zinazozozaniwa.

Mshindi ni lazima apate 50% ya kura pamoja na moja. Tume ina siku saba kutangaza matokeo baada ya kura kupigwa.

XS
SM
MD
LG