Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:38

Salamu za pongezi zatolewa na viongozi mbalimbali kwa Rais Mteule wa Kenya, William Ruto


Rais Mteule wa Kenya William Ruto
Rais Mteule wa Kenya William Ruto

Risala za pongezi zimetolewa kwa rais mteule wa Kenya  William Ruto ambaye ametangazwa mshindi wa kinyan'anyiro kilichokuwa na ushindani mkali.

Risala za pongezi zimetolewa kwa rais mteule wa Kenya William Ruto ambaye ametangazwa mshindi wa kinyan'anyiro kilichokuwa na ushindani mkali.

Rais Emmerson Mnagagwa alikuwa kati ya viongozi wa kwanza kutuma salamu za pongezi kwa rais huyo mteule.

Rais wa Somalia na Waziri mkuu wa Ethiopia pia walituma salamu za heri.

Ruto amechaguliwa kama rais wa tano wa nchi hiyo, kufuatia siku sita za uhakiki wa kura, zoezi amabalo lililosababisha hali ya taharuki na rabsha za hapa na pale.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC, Wafula Chebukati alimtangaza mshindi Jumatatu jioni katika ukumbi wa Bomas of Kenya, nje kidogo ya mji mkiuu, Nairobi.

Ruto alipata kura milioni 7,176, 141 ambayo ni asili mia 50.49 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu, mwanasiasa mkongwe, Raila Odinga aliyepata kura milioni 6,942,930, sawa na asili mia 48.85 ya kura zote.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Ruto alimshukuru Odinga kwa"kuendesha kampeni tulivu ya kunadi sera."

"Hakuna aliyeshindwa katika uchaguzi huu. Nitawatumikia Wakenya wote," Ruto aliambia waliohudhuria hafla hiyo, ambayo ilisusiwa na mpinzani wake wa karibu.

Awali hali ya wasiwasi ilitanda kwenye ukumbi huo pale ilipodhihirika kwamba Odinga hangehudhuria hafla hiyo, baada ya mawakala wake kusema kulikuwa na dosari katika uhakiki wa kura.

Hayo yalijiri huku baadhi ya makamishna wakiitisha kikao na waandishi wa habari na kusema kwamba hawakukubaliana na jinsi uhakiki huo ulivyofanyika.

XS
SM
MD
LG