Ameamuru kusitishwa vikao vya kawaida vya bunge la Agosti, na mabunge ya kwenye kaunti za Nairobi, Machakos, Kajiado, Kiambu na Nakuru na kamati zake zote.Katazo la kutoka nje usiku
Muda wa kutotoka nje usiku nchi nzima umerekebishwa kwa maeneo husika ikiwemo Kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado na Nakuru, na sasa amri hiyo itaanza kutekelezwa saa mbili usiku hadi saa kumi Alfajiri.
Amri ya kutotoka nje usiku maeneo mengine nchi nzima itakuwa kama ilivyokuwa awali, na hivyo ni kuanzia saa nne usiku.
Wanafunzi kutohudhuria madarasani
Rais Kenyatta ameamrisha kusitishwa mahudhurio ya wanafunzi madarasani katika vyuo vyote ikiwemo vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya ufundi. Ila tu kwa wale wanaofanya mitihani ya mwisho ya kumaliza masomo na wale katika vyuo vya afya hadi tamko litakapotolewa.
Kusitishwa Michezo
Shughuli zote za michezo zimesitishwa ikiwemo ile inayoendeshwa na wanachama wa vilabu hivyo.
Katazo la Mabaa na Uuzaji wa Pombe
Kenyatta pia ametoa amri ya kusitishwa biashara za kwenye baa katika kaunti 5 zilizoathiriwa zaidi na Covid-19 kuanzia saa sita usiku. Pia sitisho hilo la biashara za mabaa litatekelezwa Nairobi,
Shughuli za Kwenye Migahawa
Kadhalika uuzaji wa Pombe katika maeneo ya migahawa katika kaunti tano umepigwa marufuku. Na pia migahawa katika maeneo hayo hivi sasa yatauza vyakula na wateja watakiwa kuvichukua majumbani na siyo kula ndani ya migahawa.
Migahawa katika maeneo mengine ya nchi itaendelea kutoa huduma kama kawaida kwa kufuata miongozo ya afya ya umma.