Jeshi la Uganda limesema limemuua kamanda wa kikosi cha kundi la waasi la Islamist rebel Allied Democratic Forces (ADF) wanaoshutumiwa kufanya mauaji mabaya ikiwemo mauaji katika shule ya bweni.
Kiongozi wa huyo wa ngazi ya juu wa kundi hilo Musa Kamusi, aliyekuwa katika orodha wa watu wanaotafutwa- ameuawa katika operesheni zilizofanyka katika mbuga ya wanyama ya Kibale, ambayo ni msitu ulioko Magharibi mwa Uganda jirani na mpaka wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, msemaji wa Jeshi Deo Akiiki alisema.
Mamlaka zimekuwa zikikishutumu kikosi cha Kamusi kwa mauaji ya wanafunzi 37 katika shule iliyopo karibu na mpakani mwezi Juni, na maharusi kutoka Uingereza na Afrika kusini walikuwa kwenye mapumzikoni baad ya harusi yao na kiongozi wao wa msafara ambaye alikuwa raia wa Uganda mwezi Oktoba.
“Majeshi yetu wamekuwa yakivisaka vikosi vya ADF katika msitu Kabale… wameweza kumuua mmoja wa viongozi wanaoshukiwa wa ADF,” Akiini alisema katika taarifa ya Jumatano jioni.
Hakotoa maelezo zaidi, lakini Caleb Weiss, wa taasisi ya Bridgeway na mtaalamu wa masuala ya ghasia za kisiasa katika bara la Afrika aliandika kwenye mtandao wa X, inasemekana mapema siku hiyo hiyo ilipotokea.
“Bado haijathibitishwa, lakini ni wazi kwamba ni muhimu kwa usalama wa (Uganda) Magharibi kama itakuwa kweli” aliandika Weiss.
AFD ilikula kiapo cha kuliunga mknono kundi la waasi wa Islamic State miaka minne iliyopita. na kuendana na ongezeko kubwa la mashambulizi mabaya ya raia, hata hivyo wataalamu wa umoja wa mataifa wamesema hawajapata uthibitisho kamili wa kamada wa kundi Islamic States kuongoza oparesheni za kundi hilo la uasi.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters