Jeshi la Israel limetangaza “sitisho la kimkakati” jana Jumapili katika mapigano ya nyakati za mchana kuzunguka njia ya muhimu ya upitishaji misaada huko Gaza. Mpango huo una upungufu wa sitisho kamili la mapigano ambao ulielezewa na Rais wa Marekani, Joe Biden.
Jeshi la Ulinzi la Israel limetoa kanda ya video mwishoni mwa wiki ikidaiwa kuonyesha vitengo maalum vikifanya uvamizi kwa kile kilichoelezewa kuwa “miundo mbinu ya kigaidi” huko Gaza kukiwemo na “idadi kubwa ya silaha.”
VOA na AP hawakuweza kupata uthibitisho huru kuhusu hili au maelezo mengine ya IDF.
Uvamizi wa IDF
Uvamizi huo wa IDF ni tukio la karibuni katika mzozo wa Israel na Hamas, ambao hivi sasa umeingia mwezi wa tisa, kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Hamas ya Oktoba 7 kwa Israel. Kundi hilo ambalo limetajwa na Magharibi kuwa la kigaidi lilivuka mpaka na kuingia Israel na kuua watu 1,200 na kuwateka kiasi cha 250.
Tangu wakati huo, Israel imejibu kwa mashambulizi makali sana kwenye maeneo ya Wapalestina na kuua zaidi ya watu 37,000 wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa Wizara ya Afya inayoendeshwa na Hamas.
Umoja wa Mataifa kwa miezi kadhaa imeonya juu ya “janga” na “njaa” huko Gaza wakati Israel ikiziba njia zote muhimu za kupitisha chakula, maji, mafita na dawa ambazo kwa kawaida ndiyo zilizokuwa zikitumika.
Lakini hadi jana Jumapili, IDF ilitangaza “sitisho la kimkakati” la wakati wa mchana katika mashambulizi yake ya kijeshi kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Kuanzia saa kumi na moja asubuhi mpaka saa kumi alasiri, mpaka itakapotangazwa tena, sitisho hilo linalenga kutoa njia salama kwa magari ya misaada ambayo yanafikisha mahitaji muhimu sana yanayohitajika huko Gaza.
Ni habari njema kwa makundi ya misaada ambayo yanajitahidi kwa miezi kadhaa kufikisha bidhaa za kuokoa maisha.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani
Carl Skau wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani:“Hapa kwa kweli, tuna janga la ulinzi na maji na hali ya usafi wa vyoo ni hatari. Kama unavyojua, watu wameweka kambi mitaani, kwenye ufukwe, wengine labda na aina fulani ya kujihifadhi. Lakini, unajua, tunaendesha kupitia kwenye mito yenye maji machafu.”
Habari ya “sitisho la kimkakati” limekuja wakati serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu imetangaza kufariki kwa wanajeshi wake wanane katika mapigano huko Rafah eneo la Ukanda wa Gaza katika kile ambacho kimetajwa kuwa shambulizi baya sana kufanya na Hamas katika miezi kadhaa.
Netanyahu amelaumu vifo hivyo na bomu la kutegwa kando ya barabara au kombora.
Maandamano ya Waisraeli
Wakati huo huo, Waisraeli waliendelea na maandamano yao ya kila wiki dhidi ya serikali ya Netanyahu wakiwataka wote kumaliza vita na kuwaachia huru mateka waliochukuliwa na Hamas.
Habari za kuweka muda maalum kwa misaada ya kibinadamu inayofika huko wakati Waislamu wakisherehekea sikukuu ya Eid Al Adha, au funga maalum. Inaleta maana mpya mwaka huu, kufuatia miezi kadhaa ya vita, ambako badala ya kusherehekea katika majumba yao, Wapalestina wengi hivi sasa wanasali juu ya milima yam awe na vifusi.