Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 22:33

Israel yaendelea na mashambulizi ya Gaza Jumapili


Kifaru cha jeshi la Israel kikisogea katika eneo la kusini mwa Israel linalopakana na Ukanda wa Gaza. Picha na RONALDO SCHEMIDT / AFP.
Kifaru cha jeshi la Israel kikisogea katika eneo la kusini mwa Israel linalopakana na Ukanda wa Gaza. Picha na RONALDO SCHEMIDT / AFP.

Mashambulizi zaidi yameripotiwa Jumapili huko Gaza, siku moja baada ya majeshi ya Israel kuwaokoa mateka wanne, kwenye operesheni iliouwa takriban wapalestina 274, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Operesheni ya uokoaji ilifanyika kwenye eneo la makazi lenye watu wengi katika kitongoji cha mji wa Nuseirat, msemaji wa jeshi la Israel amesema. “Israel haitajisalimisha kwa magaidi.” Amesema waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akiongeza kuwa,” Hatutasita hadi tumalize operesheni zetu na kuwarejesha mateka wote, wakiwa hai au wakiwa wamekufa.”

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema kuwa operesheni hiyo ilikuwa na changamoto nyingi. “ Wanajeshi wa Israel walifanya operesheni hiyo wakati wakishambuliwa vikali kwenye eneo la mji ndani ya Gaza,” amesema kupitia taarifa, akiitaja operesheni hiyo kuwa ya kipekee ambayo ameishuhudia ndani ya miaka 47 ambayo amekuwa kwenye ulinzi wa Israel.

Maafisa wa afya wa Nuseirat wametaja operesheni hiyo kuwa mbaya zaidi tangu mapigano hayo yalipoanza, kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters. Maafisa wa afya wa Gaza leo Jumapili wametaja idadi ya vifo kuwa 274 kutoka 210 vilivyotangazwa awali.

Forum

XS
SM
MD
LG