Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:38

Mahakama ya Israel yaongeza muda wa Al Jazeera kutorusha matangazo nchini humo


Jengo la makao makuu ya Al Jazeera, Doha, Qatar
Jengo la makao makuu ya Al Jazeera, Doha, Qatar

Mahakama ya Israel Ijumaa imethibitisha, na kuongeza muda wa siku 35 kwa  serikali kufunga kituo cha  televisheni  cha Al Jazeera, chenye makao yake  Qatar, wizara ya sheria imesema .

Al Jazeera ambayo hutangaza kwa lugha ya Kiarabu na Kiingereza, huduma zake zilizimwa nchini Israel kwa muda wa siku 45 kuanzia mapema mwezi uliopita. Serikali ya waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu kwa muda mrefu imekuwa na mgogoro na Al Jazeera, lakini hali hiyo imekuwa mbaya zaidi baada ya kuzuka vita vya Gaza Oktoba mwaka jana.

Wizara ya sheria imesema mahakama ya wilaya ya Tel Aviv imedhibitisha maelekezo ya waziri wa mawasiliano kusitisha urushaji habari wa kituo hicho cha utangazaji cha Al Jazeera, kufunga ofisi zake nchini Israel, kuzuia fursa ya kuingia kwenye tovuti zake na kukamata vifaa vyake.

Ufungaji huo hauathiri matangazo kutoka eneo linalokaliwa kimabavu na Israel huko Ukingo wa Magharibi, au Ukanda wa Gaza, ambako Al Jazeera inaendelea kutangaza kuhusu vita vya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas. Bunge la Israel, mwezi Aprili lilipitisha sheria inayoruhusu kupiga marufuku vyombo vya habari vya kigeni vinavyoshukiwa kudumaza usalama wa taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG