Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 02:40

Hamas yajibu pendekezo la kusimamisha mapigano Gaza


Hamas imejibu pendekezo linaloungwa mkono na Marekani la kusitisha mapigano Gaza kupitia wapatanishi wa Qatar na Misri.

Qatar na Misri wanaangazia majibu hayo na kuthibitisha kuendelea na upatanishi na Marekani. Marekani yenyewe inasema inatathmini majibu ya Hamas.

Kwa mujibu wa Hamas na kundi dogo la wanamgambo, wako tayari kushughulika ili kufikia makubaliano wakiweka kipaumbele kusimamishwa kabisa kwa vita.

Majibu ya Hamas yanasisitiza msimamo wake kwa makubaliano yoyote lazima yasitishe uchokozi wa Wazayuni dhidi ya watu wao, kutoa majeshi ya Israel, yajenge upya Gaza na kufikia makubaliano makubwa ya kubadilishana wafungwa afisa wa Hamas amesema.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken yuko Mashariki ya Kati kwa mazungumzo ya mpango wa kusitisha mapigano na baada ya vita vya Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG