Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 02:50

Umoja wa Mataifa wasisitiza mwito wa Hamas na Israel kusimamisha mapigano


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatatu limeongeza ujumbe wake wa mwito kwa Hamas na Israel kutekeleza makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka wa Gaza.

β€œLeo tumepiga kura kwa ajili ya amani,” balozi wa Marekani wa Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, amewaambia wajumbe wa baraza hilo kufuatia kura ya 14 - 0 za kuunga mkono azimio lililoandaliwa na Marekani linalounga mkono pendekezo la kusitisha mapigano, huku Russia ikiacha kupiga kura.

Amesema mpango huo ndio njia bora na pekee ya kumaliza vita vilivyodumu kwa miezi 8, vilivyoanza na shambulizi la kigaidi la Hamas ndani ya Israel, hapo Oktoba 7.

Russia, ilihoji iwapo Israel imetia saini kweli na kusema hakujakuwa na maelezo ya kutosha kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano kwa baraza hilo kutoa baraka zake.

Mwakilishi wa Russia, amesema baraza hilo halipaswi kutia saini makubaliano yasiyo na uhakika.

Forum

​
XS
SM
MD
LG