Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 02:50

Blinken asema kuna ishara Hamas kuunga mkono makubaliano ya Gaza


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati ) akihudhuria kikao cha pamoja huko Jodan, Picha na Alaa AL-SUKHNI / POOL / AFP.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (katikati ) akihudhuria kikao cha pamoja huko Jodan, Picha na Alaa AL-SUKHNI / POOL / AFP.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alisema Jumanne kwamba azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa la kuunga mkono pendekezo la sitisho la mapigano huko Gaza ni ishara wazi kabisa kwamba dunia inaunga mkono mpango huo.

Hamas imekubali na iko tayari kufanya mashauriano, afisa mwandamizi wa kundi la wanamgambo la palestina alisema jumanne kwa kile ambacho Blinken ameita ni ishara ya matumaini.

Blinken amesema,

“ninasema ni ishara ya matumaini kama taarifa waliyoitoa baada ya rais kutoa pendekezo lake siku 10 zilizopita , inaleta matumaini , lakini sio ya uhakika. Kinachopingana”

Mashauriano kuhusu mipango ya Gaza baada ya vita vya Israel na Hamas kuisha yataendelea jumanne mchana na katika siku chache zijazo, waziri wa huyo wa mambo ya nje wa marekani Anthony Blinken alisema Tel Aviv baada ya mazungumzo na viongozi wa Israel.

Mchana wa leo Blinken alikua Amman Jordan ambako ametangaza msaada wa dharura wa zaidi ya dola milioni 40 kwa ajili ya Wapalestina wa Gaza.

Wakati huo huo, Mfalme Abdullah wa Jordan amesema Jumanne kwamba kuruhusu msaada wa dharura kuingia Ukanda wa Gaza hauwezi kusubiri usitishaji mapigano na hauwezi kutumia kama ajenda ya kisiasa.

Akizungumza kwenye kikoa cha ufunguzi cha mkutano wa kuchangisha msaada wa dharura kwa ajili ya Gaza ulotayarisha na Jordan, Misri na Umoja wa Mataifa, Mfalme Abdullah alisisitiza umuhimu pia wa kudhibiti mivutano kwenye ukingo wa Magharibi ili kuepusha kupanuka kwa mapigano.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaehudhuria mkutano huo ametoa wito kwa pande zote zinazohusika na ugomvi kati ya Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano chini ya mpango uliopendekezwa na rais Joe Biden.

Forum

XS
SM
MD
LG