Vikosi vya usalama vya Israel vimesema vifaru vyake na kikosi cha ardhini vilishambulia maeneo kadhaa ya magaidi, miundombinu na vituo vya kurushia makombora kabla ya kurejea katika Israel.
IDF imesema operesheni hiyo ilifanyika kwa ajili ya kujiandaa na hatua inayofuata ya mapambano.
Maafisa wa Israel wameapa kuhakikisha kwamba wanamgambo wa Hamas hawawezi tena kufanya mashambulizi yanayoitishia Israel kufuatia shambulizi la Oktoba 7 lililotekelezwa na wanamgambo lililouwa takriban watu 1,400.
SOT: Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel amesema: “ Tutakapoingia Gaza, kuendelezaz mapigano tutawashughulikia kikamlifu wauaji. Wahusika wa ukatili wa kutisha wa wanamgambo wa Hamas- ISIS. Natoa wito tena kwa watu wasiohusika na Gaza kuhamia kusini mwa ukanda wa Gaza.
Rais wa marekani Joe Biden alionyesha uungwaji mkono wake jumatano kwa kile ambacho kinaonekana sasa ni lengo kutoka mbali, matakwa ya muda mrefu ya Marekani kwa mataifa tofauti yanayojitawala ya Israel na palestina.
Biden alisema katika Mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa Australia kwamba utashi wa palestina hauwezi kupuuzwa . waisraeal na wa-palestina wanastahili kuishi pamoja , kwa usalama , utu, na amani.
Naye Rais wa Marekani Joe Biden alikuwa na haya ya kusema: "Israel ina haki na nitaongeza kwa uwajibikaji kujibu mauaji ya watu wake. tutahakikisha kwamba Israel ina kila inachohitaji kujitetea yenyewe dhidi ya magaidi hawa. Hilo ni la uhakika. pia ni lazima tukumbuke kwamba wanamgambo wa Hamas hawawakilishi, wacha mimi niseme tena, Hamas hawawakilishi watu wengi wa Palestina huko Ukanda wa Gaza au kwingineko. Hamas ni kundi la wanamgambo linalojificha nyuma ya raia wa Palestina na linachukiwa, halishangazi na ni waoga pia.”
Biden pia alieleza wasiwasi kuhusu usalama wa mateka zaidi ya 200 baadhi yao wanaaminika kuwa ni Wamarekani, waliotekwa na wanamgambo wa Hamas Oktoba 7.