Rawat anataka kuhakikisha kuwa “Imetengezwa India” kauli mbiu inayopendelewa zaidi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, inakuwa ukweli.
“Sisi siyo majeshi ya kulinda amani ambayo yanapaswa kupelekwa duniani kote,” Rawat ameliambia The Times. “Kwa hiyo, hatutakiwi kuagiza kiwango kikubwa ambacho hakifanani na mahitaji ya operesheni zetu.”
India, kama ilivyo maeneo mengine ulimwenguni, inakabiliana na matatizo ya kifedha yanayotokana na janga la COVID-19.
Ni Saudi Arabia pekee inayoipiku India katika ununuzi wa silaha za kigeni, gazeti hilo limeelezea katika ripoti yake.
Rawat amesema India inalazimika kusaidia viwanda vya ulinzi vya ndani hata kama silaha wanazo zitengeneza zinafanya kazi kwa “viwango vilivyo punguzwa kiufundi.”
“Tunatakiwa tujigambe ‘Imetengenezwa India’ kwa kuunga mkono viwanda vyetu vya ndani, hata kama inatoa silaha zenye kukidhi viwango kwa asilimia 70 katika uzalishaji wake wa awali,” Jenerali huyo amesema.