Katika hotuba kwa taifa ambayo haikutarajiwa, Modi ametaja hatua hiyo kuwa mafanikio makubwa katika uwezo wa nchi hiyo kujilinda dhidi ya silaha zozote kutoka angani.
Kombora lililovurumishwa kutoka mashariki mwa India, liliangushwwa na satellite, umbali wa kilomita 300 katika operesheni ya mazoezi yaliyochukuwa muda wa dakika tatu.
Modi amesema zoezi hilo halina lengo lolote la kutengeneza mazingira ya kivita, akituma ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa kwamba zoezi hilo haliilengi nchi yeyote.
Modi amesisitiza kwamba nia yake ni kuimarisha ulinzi wa India inayokua kwa mwendo wa kasi.
India ni nchi ya nne baada ya Marekani, China na Russia kutangaza kuwa na uwezo wa kutengeneza mitambo ya kunasa silaha zinazorushwa kuelekea katika ardhi yake.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC