Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 06:22

India : Mahakama yaruhusu wanawake kuingia Hekalu la Wahindu


Wanaume wakiongea na wanawake wawili walioingia katika hekalu la Sabarimala huko Pathanamthitta, Kerala, India, Januari 2, 2019.
Wanaume wakiongea na wanawake wawili walioingia katika hekalu la Sabarimala huko Pathanamthitta, Kerala, India, Januari 2, 2019.

Maandamo yamefanyika Jumatano katika jimbo la kusini mwa India la Kerala baada ya wanawake wawili kuingia hekalu la Wahindu na hivyo kuvunja moja ya miiiko ya karne za zamani unaokataza wanawake walo vunja ungo kuingia ndani ya hekalu hilo takatatifu.

Polisi wametumia mabomu ya machozi ya machozi kuwatawanya waandamanaji wenye hasira katika mjii wa Thiruvananthapuram saa chache baada wanawake hao wawili wenye umri ya miaka 40 kuingia ndani ya hekalu la Sabarimala, wakisindikizwa na askari polisi, ikiwa ni ukiukaji wa miiko ya dini hiyo ya Kihindu.

Mahakama nchini humo imetoa uamuzi wa wanawake kuruhusiwa katika hekalu na kutekelezwa kwa usimamizi wa polisi.

Maandamano yameripotiwa tena katika miji mingine ya jimbo la Kerala.

Historia ya nchi hiyo ni kuwa wanawake walio na umri wa kati ya miaka 10 na 50 walipigwa marufuku kuingia hekalu la Sabarimala,

Hilo linatokana na imani za waumini wa dhehebu hilo la Hindu kwamba wanawake hao wanaweza kuingiza najisi eneo hilo takatifu.

XS
SM
MD
LG