Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:28

India yapiga marufuku tamko 'nimekupa talaka' tatu


Jengo la bunge la India
Jengo la bunge la India

Nchini India juhudi za kupitisha sheria kufanya kitendo cha kutoa talaka papo kwa hapo katika jumuiya za Kiislam kuwa ni kosa la jinai limeibua malumbano makubwa.

Wakati huo huo vyama vya upinzani vimekuwa vikishawishi kupingwa kwa katazo hilo wakisema linaweza kutumika vibaya kuwanyanyasa wanaume.

Lakini wanaharakati wanawake wanatarajia vyama vya kisiasa vitaondosha hitilafu zao na kuwezesha kile kinachoonekana kitasaidia kuleta mageuzi muhimu katika sheria ya Familia za Kiislam.

“Bila shaka tunahitaji sheria hiyo. Hatua hii imechelewa kuchukuliwa baada ya miaka 70 tangia kupatikana uhuru, amesema Zakia Soman, wa kikundi cha Wanaharakati wa Bharatiya Muslim Mahila Andolan, ambacho kilikuwa ni moja kati ya wale waliokuwa mstari wa mbele katika kampeni ya kupigania sheria hiyo katika Mahakama ya Juu, wakishambulia tendo hilo la talaka ambalo liko kwa takriban karne moja, wakisema uko kinyume cha katiba miezi mitano iliyopita.

India hivi karibuni ni kati ya nchi kadhaa ambazo zimefuta sheria ya Kiislam ambayo inaruhusu wanaume wa Kiislam kuwaacha wake zao kwa kutamka neno “nimekupa talaka” mara tatu.

Lakini kusema kuwa utamaduni huo unaendelea pamoja na kuwepo amri ya mahakama na serikali imeanzisha muswada kufanya kitendo cha kutamka “talaka tatu” ni kosa lisilotolewa dhamana na adhabu ya miaka mitatu jela. Sheria hiyo ilipitishwa kwa urahisi Disemba mwaka jana katika baraza la chini la bunge.

Hata hivyo wabunge wa upinzani wa baraza la juu la bunge la nchi hiyo wiki iliyopita waliweka pingamizi wakisema pendekezo la kifungo kwa wanaume ambao wanaamua kutumia utamaduni wa miaka mingi kuvunja ndoa zao inajichukulia madaraka kwa kufanya kile ambacho kwa hakika ni makataba binafsi kuwa sheria ya jinai.

Wanasema kuwa kipengele hicho cha kumpata mwenye makosa aendelee kumsaidia mkewe haina mantiki yoyote kwani hawezi kumsaidia mwanamke huyo akiwa Jela.

Washabiki wa muswada huo wanatetea vifungu hivyo vigumu wakisema kuwa msimamo mkali zaidi unahitajika kuzuia wanaume wa Kiislam kuamua mara moja kutamka "talaka tatu".

XS
SM
MD
LG