Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:38

India yawanyonga wahalifu wanne wa ubakaji, mauaji


Asha Devi (katikati), mama wa muhanga wa unyama wa ubakaji uliotokea 2012 New Delhi, India akionyesha alama ya ushindi baada ya hukumu Machi 20, 2020. (Foto: AP)
Asha Devi (katikati), mama wa muhanga wa unyama wa ubakaji uliotokea 2012 New Delhi, India akionyesha alama ya ushindi baada ya hukumu Machi 20, 2020. (Foto: AP)

Watu wanne wamenyongwa Ijumaa, miaka saba baada ya kukutikana na makosa ya ubakaji wa kinyama wa pamoja na mauaji ya mwanafunzi wa miaka 23 mjini New Delhi.

Kesi hiyo ilianza kumulika vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake nchini India. Wanawake katika mji huo mkuu wa India, wametaja kuwa mji huo ni moja ya miji isiyokuwa salama duniani, na hali bado haijatengemaa.

Maandamano kufuatia kitendo hicho cha kinyama cha ubakaji wa mwanamke mwenye umri wa miaka 23 katika mji mkuu wa India mwaka 2012 ndani ya basi kumetoa shinikizo kuwepo ulinzi zaidi kwa wanawake. Miaka saba imeshapita lakini vitendo vya uhalifu wa ngono haujaweza kuzuiliwa.

Mwandishi wa maudhui Varsha Kar anasema : “Haikubaliki. Takriban kila siku, kuna tukio la habari zinazoongelea ubakaji mpya. Sidhani kama kuna mabadiliko hata kidogo.”

Aastha Sharma, Meneja wa Kampuni ya Kusambaza Chakula anasema : “Bado tunasikia matukio kama hayo (ya ubakaji) kila wiki, kila mwezi, na kila mwaka.”

Kutokana na hofu ya kutokuwepo usalama barabarani, wanawake lazimi wawe makini wanaposafiri, hususan wakati wa usiku, amesema mwandishi wa habari za chakula na safari, Ayandrali Dutta.

“Naelewa, lazima uhakikishe hakuna gari, pikipiki, hakuna kitu chochote kinachokufuata. Siku zote lazima nipige simu na kuongea na mtu nikiwa safarini kuhakikisha usalama wangu.”

XS
SM
MD
LG