Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:34

Mkutano wa Asia Mashariki waanza Bankok


Viongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya kiuchumi ya Asia Kusini, ASEAN, wakutana Thailand, Novemba 4, 2019. REUTERS/Athit Perawongmetha - RC14824166D0
Viongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya kiuchumi ya Asia Kusini, ASEAN, wakutana Thailand, Novemba 4, 2019. REUTERS/Athit Perawongmetha - RC14824166D0

Viongozi wa nchi za Jumuia ya Asia Mashariki wamefungua rasmi mkutano wao wa 14 mjini Bankok, Thailand, Jumatatu wakiungana na viongozi kutoka jumuiya ya maendeleo ya kiuchumi ya Asia Kusini, ASEAN.

Viongozi wa ASEAN walimaliza mkutano wao wa 35 wa siku tatu leo huko mjini Bankok kwa kutangaza makubaliano juu ya mikataba minne muhimu ya biashara kati ya jumuia hiyo yenye wajumbe 16 .

Akizungumza na waandishi habari hii leo baada ya kumalizika kwa mkutano wa ASEAN waziri mkuu wa Thailand Prayuth Chan-Ocha amesema huu ulikuwa mwaka wa mafanikio kwa jumuia hiyo iliyoweza kujenga misingi endelevu ya ushirikiano kwa miaka ijayo.

Waziri Mkuu Chan Ocha alimkabidhi uenyekiti unaobadilika kila mwaka wa Jumuia hiyo kwa Waziri Mkuu wa Vietnam Nguyen Xuan Phuc ambaye amepongeza mafanikio hayo muhimu.

Waziri Mkuu wa Vientam

Kwa hakika ni nafasi nzuri sana kwa Vietnam kuchukua uwanachama wa ASEAN kwa mwaka 2020, ambao utaadhimisha miaka 5 tangu jumuia hiyo kuweka misingi madhubuti ya maendeleo kwa miongo mitano ijayo. Wanachama wa ASEAN wataendelea kukuwa pamoja kiuchumi kihistoria na kiutamaduni kwa faida ya wakazi wake.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amepongeza maendeleo yaliyofikiwa ambapo viongozi wamesema wanatarajia kutia saini mkataba muhimu wa biashara huru RECP utakaounda Jumia kubwa kabisa ya biashara dunia.

Jumuia hiyo ya kikanda inaungwa mkono nachina na inawajumuisha pia wanachama 10 wa ASEAN pamoja na Korea Kusini, japan india Australia na New Zealand.

Mvutano kati ya Marekani na China

Mkataba huo umepata umuhimu mkubwa kutokana na vita vya biashara kati ya Marekani na China, ambapo nchi za Asia zinahisi kuna haja ya kuwepo na Jumiya yenye nguvu ya biashra huru pindi kuna matatizo kati ya mataifa makuu ya biashara duniani.

Licha ya kwamba Rais Trump hakuhudhuria mkutano huo waziri wa biashara wa Marekani Wilbur amesisitiza kwamba nchi yake inaendelea kujihusisha kwa dhati katika ushirikiano na nchi hizo za Asia.

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Robert O Brien amesema Marekani itawasaidia marafiki zake wa ASEAN kutetea uhuru wake akiituhumu China kutaka kupanua nguvu na ushawishi wake katika kanda hiyo.

Ameongeza kuwa kanda hii haina haja ya kuwa na enzi mpya ya ubeberu ambapo nchi kubwa inaweza kuwatawala wengine. Marekani iko tayari kuwasaidia marafiki zake wa ASEAN kulinda uhuru wa mipaka yake.

Viongozi 7 kati ya 10 waliamua kususia mkutano wa tatu wa viongozi kati ya nchi za Asia kusini na Marekani hii leo huko Bankok kutokana na Rais Trump kutohudhuria mkutano wa ASEAN and ule wa nchi za Asia Mashariki ulofunguliwa hii leo.

Mkutano huo wa 14 wa nchi za Asia Mashariki unatarajiwa kuzungumzia zaidi juu ya masuala ya biashara kati ya nchi zao ugomvi wa biashara kati ya China na Marekani na masuala mengine ya kimataifa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG