Mashambulizi hayo yameathiri ulinzi wa anga wa Syria lakini hayaja sababisha mauaji, shirika la habari la serikali ya Syria limeripoti, ni shambulizi la pili katika zaidi ya wiki mbili.
Jeshi la Israeli lilikataa kutoa maoni juu ya ripoti hiyo.
Chanzo cha jeshi la Syria kilichonukuliwa na chombo cha habari cha serikali kilisema mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria uliangusha makombora mengi ya Israeli.
Imeongeza kuwa lakini ni uharibifu wa vifaa pekee ndiyo uliofanyika katika shambulizi hilo la saa 7 usiku.
Israeli imekuwa kwa miaka kadhaa ikiendeleza mashambulizi juu ya kile ilichoelezea kama malengo yaliyo na uhusiano na Irani huko Syria.
Israeli inasema vikosi vinavyoungwa mkono na Tehran ikiwa ni pamoja na Hezbollah ya Lebanon vimejikita huko tangu kupelekwa kumsaidia Rais Bashar al-Assad katika mzozo wa Syria uliyoibuka mwaka 2011 .