Katika ufunguzi huo wawakilishi wake walisifu fursa za biashara na uwekezaji ambazo ushirikiano huo utaweza kuleta.
Wakati wa ufunguzi wa ofisi hiyo rais wa Israeli alihudhuria.
Yakiwa yameunganishwa pamoja na hali tete ya Iran, mataifa ya UAE na Bahrain yalianzisha uhusiano wa kawaida na Israel mwaka 2020, chini ya mkataba wa Abraham ulioandaliwa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump.
Nazo Sudan na Morocco pia zimeelekea kuanzisha ushirikiano na Israel. Kufunguliwa kwa ubalozi wa UAE, ambao unapatikana Tel Aviv, umezinduliwa baada ya kuzindiliwa ubalozi wa Israel nchini UAE mwezi uliopita.
Rais wa Israel Isaac Herzog ameuita ufunguzi huo wa ubalozi kuwa ni hatua muhimu katika safari ya kuelekea wakati ujao wenye ustawi wa amani, Salama katika Mashariki ya Kati.