Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:04

Israel imefungua ubalozi wake mjini Abu Dhabi


Yair Lapid akizungumza baada ya kuzindua ubalozi mpya Abu Dhabi
Yair Lapid akizungumza baada ya kuzindua ubalozi mpya Abu Dhabi

Lapid akiwahutubia mabalozi wa nchi za kigeni waliohudhuria sherehe hizo amesema huu ni wakati wa kihistoria na kwamba Israel inahitaji kuwa na amani na majiani zake wote kwani Mashariki ya kati ni nyumbani kwao

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel Yair Lapid amefungua ubalozi wa kwanza wa Israel katika nchi za Ghuba mjini Abu Dhabi siku ya Jumanne wakati akianza ziara ya kihistoria katika umoja wa falme za kiarabu.

Akiwahutubia mabalozi wa nchi za kigeni waliohudhuria sherehe hizo amesema huu ni wakati wa kihistoria na kwamba Israel inahitaji kuwa na amani na majiani zake wote kwani Mashariki ya kati ni nyumbani kwao.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken alipongeza kufunguliwa kwa ubalozi huo. Ziara hiyo ya Lapid ni ya kwanza kufanywa na afisa wa cheo cha juu wa Israel huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) miezi tisa baada ya nchi hizo mbili kuanzisha tena uhusiano kati yao.

Mazungumzo ya Lapid na mwenyeji wake Sheikh Abdullah bin Zayed yanatarajiwa kuzingatia juu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, masuala ya mashariki ya kati, na suala la Iran, nchi ambayo mataifa hayo mawili yanaichukulia kuwa ni kitisho kwa kanda nzima.

XS
SM
MD
LG