Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:22

Afrika Kusini yapinga hatua ya AU kuipa Israeli hadhi ya Uangalizi


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Afrika Kusini imepinga vikali uamuzi wa pekee wa wiki iliyopita uliofanywa na tume ya Umoja wa Afrika kuipa Israel hadhi rasmi ya kuwa mwangalizi, katika taasisi ya bara hilo.

Katika taarifa yenye maneno makali, ambapo mwaka jana walipata hadhi ya urais wa AU nafasi ambayo ni ya kupokezana, Afrika Kusini imesema imesikitishwa sana na uamuzi ambao si mzuri, uliofanywa na tume ya AU, kuipa Israel hadhi ya uangalizi katika Umoja wa Afrika

AU iliipa Israel hadhi hiyo Alhamisi, hatua ambayo pande hizo zilitarajiwa kuiwezesha Israel kuisaidia zaidi AU, katika mapambano yake ya janga la virusi vya corona, na ugaidi kwenye bara hilo.

Uamuzi wa kuipa Israel hadhi hiyo unashtusha Zaidi, katika mwaka ambbao ukandamizaji wa watu wa Palestina ulisababisha uharibifu mkubwa kwa kuwapiga mabomu na kuendelea kukalia ardhi yao, kimabavu, wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imesema, ikishutumu vikali, na kusema kuwa ni jambo lisiloelezeka na lisiloeleweka.

XS
SM
MD
LG