Moto huo umeendelea kuwaka katika eneo la mlima kilimanjaro kwa siku tano sasa.
kwa mujibu wa Waziri wa Utalii Hamisi Kigwangalla, wafanyakazi wa Wazima moto na wanaojitolea "wanahangaika", kuzima moto huo ambapo juhudi za kuudhibiti bado hazijafanikiwa kabisa.
Hata hivyo inaelezwa kuwa upepo mkali, vichaka vikubwa na nyasi kavu vinakwamisha maendeleo ya kazi ya kuzima moto. Zaidi ya watu waliojitolea 500 wamekuwa wakipambana na moto kwenye mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.
Ingawa chanzo cha moto hakijulikani, Mamlaka ya Hifadhi za Kitaifa ilisema kulikuwa na dalili kwamba inaweza kusababishwa na watu ambao walikuwa wanapika katika eneo la kupumzika mlimani.