Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:47

Polisi wasema Tundu Lissu hatakiwi tena kuripoti kwao


Tundu Lissu
Tundu Lissu

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Ijumaa ilibatilisha wito wa kumtaka mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kufika kituo cha polisi.

Katika barua yao Jeshi la Polisi badala yake lilimtaka aendelee na ratiba za kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2020.

Barua iliyokuwa imetumwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ilimtaka Lissu kuripoti polisi Ijumaa.

Polisi walikuwa wamemtaka kufika ili kuhojiwa kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi huku ikimtuhumu Lissu kugombana na wakuu wa polisi.

Awali, kupitia ujumbe wa Twitter, Lissu alikuwa amesema angeendelea na ratiba yake kama ilivyokuwa imepangwa, ikiwa ni pamoja na kukutana na mabalozi wa nchi za kigeni.

"Hiyo barua haielezi ni makosa gani nilifanya na imetumwa kwa mwenyekiti wa chama," alisema Lissu.

XS
SM
MD
LG