Mvua kubwa kutokana na hali mbaya ya hewa ya kimbunga Grace imeharibu juhudi za uokozi Jumanne.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema mvua kubwa pia zimeharibu upatikanaji wa huduma za maji, makazi , na huduma nyingi za msingi.
Hospitali katika maeneo ya kusini magharibi mwa nchi ambako tetemeko lilitokea zimeelemewa na idadi ya watu waliojeruhiwa na zinahitaji wafanyakazi zaidi wa afya na vifaa ikiwemo dawa za kupunguza maumivu.
Mexico na Jamhuri ya Dominican ni miongoni mwa nchi zilizotuma msaada wa chakula na dawa.
Cuba imepeleka wafanyakazi 235 wa huduma za afya.
Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres alisema katika taarifa Jumanne, UN ipo katika eneo la tukio huko Haiti na imetenga dola milioni 8 kutoka mfuko wa huduma za dharura kwa ajili ya kusaidia huduma za afya, maji safi, makazi ya dharura na vifaa vya usafi kwa wale wote walioathiriwa na tetemeko la ardhi.