Donald Trump aapishwa leo Jumatatu kushika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani

  • VOA News

Donald Trump aapishwa kuchukua rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

Donald Trump ameapishwa  leo Jumatatu kuchukua rasmi hatamu za uongozi kama rais wa 47 wa Marekani. Kurejea kwake madarakani ni tukio la kihistoria kwa mtu ambaye katika kipindi cha zaidi ya miaka tisa alikibadili  chama cha Republican katika nchi inayozidi kukumbwa na  migawanyiko.

Donald Trump anasema alichaguliwa tena na kupewa "mamlaka ya aina yake na yenye nguvu" na wapiga kura wa Marekani.

Donald Trump, Rais Mteule anasema: "Nataka kuwashukuru watu wa Marekani kwa heshima kubwa ya kuchaguliwa kuwa rais wenu wa 47 na rais wenu wa 45. wananchi wote. Nitakupigania, kwa ajili ya familia yako na maisha yako ya baadaye. Kila siku nitakuwa nikikupigania. kwa kila pumzi katika mwili wangu, sitapumzika hadi tutakapoikabidhi Marekani yenye nguvu, salama na ustawi, Marekani ambayo watoto wetu wanastahili na ambayo wewe unastahili."

Kurejea kwa Trump madarakani ni sehemu ya hulka yake ya kutokuwa tayari kukubali jibu la “hapana.”

Russ Buettner wa New York Times anasema: "Nadhani unachokiona ni mtu ambaye anajiamini sana katika msimamo wake mwenyewe."

Buettner na Susanne Craig ni waandishi wa habari za uchunguzi wa New York Times na waandishi wenza wa ripoti ya "Lucky Loser," inayoangazia kwa kina jinsi Trump alivyokuwa bilionea aliyejijenga mwenyewe.

Buettner anaeleza zaidi: "Tangu miaka ya mwanzoni ya 80 hajaamini kabisa uwezo wa watu ambao wana utaalam katika karibu kila kitu. Atawapuuza daima... …na kufanya mambo jinsi anavyotaka yawe.”


Majengo ya Trump yalikuwa yamepambwa kwa jina lake kwa herufi kubwa za dhahabu, kama ishara ya nia yake na kujipigia debe.
Huyu hapa Susanne Craig.

Craig wa New York Times anasema: "Alikuwa na utajiri wa dola milioni 200 wakati alipokuwa akizungumza - kulikuwa na mahojiano aliyofanya na The New York Times - na thamani yake ilikuwa hadi dola bilioni alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha '60 Minutes' muongo mmoja baadaye."


Trump alibobea katika kuvutia umakini na kujijengea umaarufu kama mfanyabiashara. Alitengeneza mamilioni katika kutangaza jina lake.
((BROLL Trump with celebs, hotels, The Art of the Deal book))
Lakini mbali na mafanikio hayo kulikuwa na matatizo. Kampuni zake ziliwasilisha hoja za kufilisika mara sita. Kasino zake zilipoteza pesa na kufungwa.


Trump alirejea na kipindi chake cha Televisheni, “The Apprentice,” ambapo alicheza nafasi kubwa zaidi kama mshiriki.


Rais Trump akihutubia alisema: "Mabibi na mabwana, ninagombea rasmi urais wa Marekani, na tutaifanya nchi yetu kuwa bora zaidi tena." Akiwa bila masikitiko na kujieleza bila kuchuja lolote, Trump alikuwa mgombea aliyeligawanya taifa, ...na mzalendo.
Trump anasema: "Wakati Mexico inapotuma watu wake, haiwatumi walio bora zaidi. Wanaleta dawa za kulevya, uhalifu, ni wabakaji, na wengine, nadhani, ni watu wazuri.
Kama rais, Trump aliteua majaji watatu wa Mahakama ya Juu ambao walisaidia kubatilisha sheria ya haki za utoaji mimba iliyoratibiwa na serikali kuu.
Mapema mwaka 2020, janga la COVID-19 lilikuwa changamoto kwa Trump. Aliweka mikakati ya haraka ya utengenezaji wa chanjo za kuokoa maisha. Lakini pia alionekana kupendekeza kwamba wanasayansi wafanye utafiti kuhusu matumizi ya kemikali za kufua nguo, maarufu bleach, katika kuua virusi.
Huku Wamarekani zaidi ya milioni 9 wakiwa wameambukizwa na idadi ya vifo ikiwa zaidi 230,000, wapiga kura Novemba mwaka huo walimchagua Joe Biden kama rais wao ajaye.
Alipoondoka madarakani, Trump alikabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhalifu na ndiye rais wa kwanza wa zamani kukutwa na hatia ya uhalifu. Lakini licha ya hayo, amepata umaarufu kuliko wakati mwingine wowote.
Kunusurika majaribio mawili ya mauaji mwaka jana...
Nats Butler anasema: ...kuliimarisha tu uhusiano na wafuasi wake.

Kama Pam Smith, wa Evans City, Pennsylvania

Smith, Mfuasi wa Trump wa Trump anaeleza: “Mungu ana mpango na Trump. aliokolewa kabisa kwa kusudi na sababu fulani. Nadhani ni ili awe rais wa 47."

Siasa za Marekani zimebadilika tangu Donald Trump aingie kwenye kinyang’anyiro.
Akiwa mtu ambaye aliyewahi kuandika kitabu kiitwacho "The Art of the Comeback" anarudi madarakani baada ya moja ya mafanikio makubwa zaidi ya kisiasa, katika historia ya Marekani.