Katika siku yake ya kwanza ofisini aliahidi kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni zake saa chache kabla ya kuapishwa baadaye Jumatatu. “ Wakati jua litakapotua kesho, uvamizi katika nchi yetu utafikia hatima yake,” Trump alisema wakati waliohudhuria kwenye ukumbi wa Capital One Arena wakimshangilia kwa maneno ya Make America Great Again.
Trump alirudia tena ahadi yake ya wakati wa kampeni ya kuwaondoa nchini mamilioni ya wahamiaji haramu, ikiwa operesheni kubwa zaidi katika historia ya Marekani. Hata hivyo , operesheni hiyo huenda ikachukua miaka kadhaa ikihusisha gharama kubwa ya fedha. Mkutano huo ulikuwa sawa na mikutano mikubwa ya kampeni ambayo imekuwa nguzo muhimu kwa Trump tangu alipowania urais kwa mara ya kwanza 2016.
Mkutano huo ni wa kwanza mkubwa kufanyika Washington baada ya ule wa 2021 ambao ulitanguliwa na uvamizi kwenye jengo la bunge uliofanywa na wafuasi wake waliokuwa na ghadhabu. Wakati wa kampeni zake mwaka jana, Trump aliahidi kutoa msamaha kwa zaidi ya wafuasi 1,500 ambao wamefungwa baada ya kukutwa na hatia ya uvamizi huo.
Trump pia ameahidi kufanya marekebisho makubwa jeshini na kwamba ataliamuru jeshi kutengeneza mfumo wa ulinzi kote Marekani ingawa hakuna maelezo ya kina ya namna hilo litakavyotekelezwa.
Forum