Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 04:25

Mwanamitindo wa Slovenia ambaye amekuwa mke wa Rais wa Marekani


Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania.
Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania.

Leo katika Dunia ya Wanawake tunamzungumzia Melania Trump. Mwanamitindo wa Slovenia ambaye amekuwa mke wa Rais wa Marekani,  amerejea White House baada ya kampeni ndefu ya mume wake Donald Trump ambaye aliapishwa jana kama rais wa 47 wa Marekani.

Rais Trump alichukua madaraka ya urais mara ya kwanza mwaka 2016. Veronica Balderas Iglesias wa VOA anatupia jicho maisha yake na matarajio ya wapiga kura kwa muhula wake wa pili. Khadija Riyami.


Wazazi wake walimpa jina Melanija Knavs. Dunia hivi sasa inamfahamu kama Mke wa Rais, Melania Trump.

Alizaliwa April 26, 1970, huko Novo Mesto, Slovenia, iliyokuwa Yugoslavia. Alipokuwa akiishi wakati wa utotoni katika mji wa Sevnica, baba yake alikuwa akiuza magari, na mama yake alifanya kazi kwenye kiwanda cha nguo.

Knavs, hata hivyo, alikuwa na utashi mkubwa sana kuwa mwanamitindo, anamkumbuka rafiki yake wa zamani alipokuwa shule, Mirjana Jelancic.

Mirjana Jelancic, Rafiki wa Utotoni anasema: “Pia alikuwa akipenda kuwa mbunifu, alikuwa akishona nguo kutoka zile za zamani.”


Knavs aliacha masomo ya chuo cha ubunifu, na kutumia jina lake Melania Knauss, aliendelea na utashi wake wa kuwa mwanamitindo huko Ulaya. Katika miaka ya 1990, mafanikio yake yamefikisha mpaka Marekani.

Profesa wa historia katika Chuo Kikuu cha Ohio, Katherine Jellison anaelezea.

Jellison wa Chuo Kikuu cha Ohio anasema: “Kama mwanamitindo na mtu ambaye mara kwa mara alikaribishwa hafla za hali ya juu huko New York, ninavyoelewa, ni kwamba huko ndiyo alikutana na Donald Trump.”

Knauss amekuwa Melania Trump Januari 22, mwaka 2005, na kujifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume Barron, mwaka mmoja baadaye. Mwaka huo huo, pia alikuwa raia wa Marekani.

Maisha ya Melania Trump yalichukua mwelekeo tofauti wakati mume wake alipowania urais wa Marekani mwaka 2016 kupitia chama cha Republican, alijiunga katika mikutano ya kampeni.

“Ni vizuri sana hapa kuwa hapa hivi leo na wewe na mume wangu. Ninajivunia sana naye.”

Donald Trump aliapishwa kama rais wa 45 wa Marekani Januari mwaka 2017.

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, Makamu wa Rais JD Vance na mkewe Usha Vance wakiwasili katika Makaburi ya Kitaifa ya Arlington, Jumapili, Jan. 19, 2025, huko Arlington, Virginia. (AP Photo/Evan Vucci)
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, Makamu wa Rais JD Vance na mkewe Usha Vance wakiwasili katika Makaburi ya Kitaifa ya Arlington, Jumapili, Jan. 19, 2025, huko Arlington, Virginia. (AP Photo/Evan Vucci)


Kama mke war ais, Melania Trump alifanya ziara duniani na kuanzisha miradi kama vile ‘Be Best’ akilenga kwa ustawi wa watoto, usalama wa kwenye mitandao, na matumizi mabaya ya dawa opioid.

Hakuwa akijiweka mbele sana kama ilivyokuwa kwa wake wengine wa marais lakini bado alikabiliwa na ufuatiliaji wa karibu sana wa vyombo vya habari, Jellison anaelezea.

Katherine Jellison wa Chuo Kikuu cha Ohio anaeleza: “Akikosolewa katika baadhi ya sehemu kuhusu uchaguzi wake wa amavani, kwa uamuzi wake wa kutohamia White House haraka, kwa kampeni yake ya ‘Be Best’ kutokuwa moja ya miradi yenye mafanikio sana ya umma ulioanzishwa na mke war ais.”

Baada ya kuondoka White House, Melania Trump kiukweli alipotea kutoka kwenye macho ya umma.

Mara kwa mara alijitokeza kuunga mkono jitihada ya mumewe katika kampeni ya mwaka 2024 ya kuchaguliwa tena.

Na kukuza kitabu cha kumbukumbu yake. Melania Trump, Mke wa Rais wa Marekani “ Kuandika kumbukumbu hii imekuwa safari binafsi na kutafakari safari yangu.”

Mpiga kura Wisconsin Austin Smith alimpigia kura Donald Trump mwaka 2016. Alielezea matumaini yake kwa Melania Trump kurejea White House.

Austin Smith, Mpiga Kura Marekani anaeleza: “Ningependa labda achukue miradi kadhaa ya Wanyama. Jambo moja ambalo ninalipenda sana ni chakula cha mchana katika shule.”

Mpiga Mdemocrat Jasleen Kaur angependa Melania Trump awe nikikariri “mke war ais mwenye athari.”

Jasleen Kaur, Mpiga Kura Marekani anasema: “Kutoka nje na kuzungumza na jamii za mijini, kutoka kote nchini, na kujifanya ujulikane, siyo tu kama mtu aliye nyuma yar ais, lakini kama mwanamke mwenye madaraka fulani.”

Mchambuzi Jellison, hata hivyo, anadhani awamu ya pili ya mke wa rais, Melania Trump kwa hakika itaendelea, kwa kiasi kikubwa, mbali na mwangaza.

Forum

XS
SM
MD
LG