Ssemakula alifariki Alhamisi asubuhi katika kituo cha afya cha Amazing Grace huko Ntungamo baada ya kupata shinikizo la damu kuongezeka.
Angalau watoto wake 64 walihudhuria maziko wakati ndugu zao wengi waliokuwa mbali na nyumbani walishindwa kusafiri kutokana na masharti ya kufasiri yaliyotangazwa na Rais Yoweri Museveni mwezi uliopita.
Takriban wajukuu zake 200, wake zake sita, na ndugu zake kadhaa na viongozi wa dini walihudhuria maziko licha ya amri ya serikali iliyoweka masharti kwa idadi ya waombolezaji katika msiba isizidi watu 20.
“Kwa sababu ya Sharia (amri ya Mungu) ilitulazimu kumzika Alhamisi Asubuhi. Wengi kati ya ndugu na watoto wake walilalamika kwa kunyimwa fursa ya kumzika baba yao,” mdogo wake Ssemakula, Daudi Suubi alimwambia mwandishi wa habari.
Baadhi ya watoto wa Ssemakula wanafanya kazi idara za usalama: polisi, jeshi na ofisi za umma, kati ya nyingine.
Issa Turyeija, mkurugenzi wa Maabara ya Mitishamba ya Ruteda amesema ametumia sehemu ya muda wake Jumatano akiwa na Ssemakula mjini Rubaare kabla ya kuchukuliwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya jioni yake.
Chanzo cha Habari : Gazeti la The Daily Monitor la Uganda