Ajali ya Lori la mafuta lililolipuka eneo la Msamvu mjini Morogogoro, Tanzania, Jumamosi saa mbili asubuhi imesababisha vifo zaidi ya watu 60.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mtafungwa amethibitisha kutokea ajali hiyo.
Majeruhi 70 waliungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta kupata ajali na kisha kulipuka moto mjini Morogoro.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa wengi wa waliopoteza uhai walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo. Pia inahofiwa kuwa kuna miili mingine ambayo imebanwa chini ya lori hilo baada ya moto kulipuka.
Rais John Mgufuli ametuma rambirambi zake kwa familia za waathiriwa na kuwatahadharisha wananchi dhidi ya kukimbilia malori ya mafuta yanapohusika katika ajali.
Morogoro ambao ni mkoa ulioko mashariki mwa Tanzania ni moja ya mikoa ambako barabara kuu za malori yanayosafirisha mizigo na mafuta hupitia.