Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:59

Polisi Kenya waanza kuchunguza ajali ya moto katika Soko la Gikomba


Soko kuu la Gikomba mjini Nairobi lawaka moto
Soko kuu la Gikomba mjini Nairobi lawaka moto

Polisi wameanza uchunguzi kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika soko la Gikomba Ijumaa na kuharibu mali zinazokadiriwa kuwa na thamani ya mamilioni ya shilingi za Kenya

Japo kiini cha moto huo hakijabainika, Rais Uhuru Kenyatta amevielekeza vyombo vya uchunguzi nchini humo kuharakisha uchunguzi huo kubaini kisababishi cha moto huo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wachuuzi wa bidhaa katika eneo hili wanasema kuwa moto huo ulianza kuteketeza vibanda vya samaki na nyama usiku wa kuamkia Ijumaa na kuendelea kuwaka saa kadhaa hadi mchana.

Soko la Gikomba ambalo ni mojawapo ya masoko makubwa mno ukanda wa Afrika Mashariki, ni maarufu kwa nguo za mitumba ambazo hununuliwa mno na watu wa kipato cha chini katika ukanda huo.

Wafanyabiashara kutoka mataifa ya kigeni hufurika soko hili kununua bidhaa kwa gharama ya chini mno.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ameripoti kuwa hii si mara ya kwanza soko hilo kuwaka moto, kila mara moto unapozuka wafanyabiashara hupoteza bidhaa zenye thamani ya mamilioni. Lakini kisa hiki cha Ijumaa kinanyooshewa kidole na baadhi ya wachuuzi ambao wanasema kuwa huenda watu fulani walichoma soko hilo kimakusudi.

Baadhi ya wachuuzi katika soko hilo walieleza Idhaa ya Sauti ya Amerika kuwa walipoteza bidhaa zao za thamani ya juu na vile vile kuiomba serikali kuwatolea ufadhili kama dhamana ya bidhaa zao zilizoteketea motoni.

Halmashauri ya kudhibiti majanga nchini Kenya sasa inawataka watu walioshuhudia kilichosababisha moto huo kufika mbele yao na kuelezea kwa kina kile walichokishuhudia.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG