Moto huo ulitokea katika eneo linalohifadhi mbao, mratibu wa mji wa Nairobi Kangethe Thuku, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu amesema.
Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa moto huo ulianza majira ya saa nane na nusu usiku na kuenea katika soko la Gikomba.
Nyumba zilizokuwa karibu na eneo hilo na vitongoji vyake ziliathiriwa vibaya sana kabla ya moto huo kudhibitiwa dakika tisini baada ya kuzuka kwake, kwa mujibu wa kituo cha Huduma za Dharura cha St John Ambulance.
Eneo hilo la Gikomba ambalo liko katikati ya mji uliokuwa na wakazi wengi, ni sehemu ya uhai wa soko la biashara isiyo rasmi, ikiwa ni mahali panapo uzwa kila kitu kuanzia mitumba mpaka thamani nyingine na mara kwa mara imekuwa ikiathiriwa na moto.