Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 06:52

Kenyatta alaumu mamlaka ya uchukuzi kwa ajili ya Naivasha


Naibu rais William Ruto akitizama mabaki ya moja wapo ya magari yaliyotekekea Naivasha katika ajali iliyosababisha vifo vya watu 40 Disemba 11, 2016.
Naibu rais William Ruto akitizama mabaki ya moja wapo ya magari yaliyotekekea Naivasha katika ajali iliyosababisha vifo vya watu 40 Disemba 11, 2016.

Rais Uhuru Kenyatta amewalaumu maafisa wa wizara ya uchukuzi kwa kuweka matuta bila ya kuweka alama ya matuta hayo barabarani.

Akihutubia wa Kenya wakati wa sherehe za 53 za uhuru wa nchi yao Rais Kenyatta amesema nchi haiwezi kupoteza maisha ya watu kwa ajili ya uzembe wa kazi.

Kiongozi huyo aliwaamrisha maafisa wa wizara ya uchukuzi kuweka mara moja alama zinazostahiki kwenye maeneo yenye matuta nan i lazima tabia ya kutotia rangi maeneo hayo lazima isitishwe mara moja.

Teknolojia ya DNA kutumika

Mwandishi wa VOA Jijini Nairobi anasema tayari miili 36 imehifadhiwa katika Hospitali ya Chiromo Nairobi and miili mingine minne ipo katika sehemu ya kuhifadhia maiti katika Hosipitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, aliiambia VOA.

Ameongeza kusema kuwa taratibu za kutambua miili ziko tayari na kuwa itatumika teknolojia ya DNA kutambua miili hiyo.

Gari hiyo mpaka sasa haijatambuliwa ni nani mmiliki wake, na hakuna habari zozote iwapo dreva wa gari hilo alisalimika katika ajali hiyo, alisema.

Hata hivyo taarifa za polisi zinaeleza kuwa watu 10 walijeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Pia Mwandishi wetu anasema mpaka hivi sasa hakuna taarifa zozote kutoka polisi juu ya kukamatwa mtu yoyote kufuatia ajali hii.

Maadai ya gari aina ya kenta ilibeba “gundi”

Mwanamke akilia baada ya kushuhudia ajali Naivasha
Mwanamke akilia baada ya kushuhudia ajali Naivasha

Wakati huo huo mwandishi wa Sauti ya amerika Kennedy Wandera anaripoti gari aina ya Kenta inasadikiwa ilikuwa imebeba “gundi” wakati ilipo gonga magari mengine na kuwaka moto katika njia kuu kati ya Nairobi na Naivasha, na tayari idadi ya waliokufa imefikia 40

Lakini taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya zinasema ni Tenka lenye kemikali ndilo lililosababisha ajali hiyo.

Mwachi Pius Mwachi, Naibu Mkurugenzi na Ofisa Mawasiliano wa Kitengo cha Kusimamia maafa cha Taifa amenukuliwa akisema “tenka hilo lilipoteza mwelekeo lilipokuwa linashuka kilima kutoka mji mkuu wa Nairobi likielekea Naivasha Jumamosi”.

“Hii ni ajali mbaya sana ya kemikali,” Mwachi alisema. Polisi na waokoaji wengine wako kwenye eneo la ajali… wakisafisha njia na kuondosha miili pamoja na magari yalikuwa yameungua.

Felestus Kioko, mratibu wa Shirika la Red Cross amesema zaidi ya miili 30 imeshapatikana.

Takwimu za ajali za barabarani

Mwachi amesema, takriban magari 11 yaliungua katika ajali hiyo. Polisi wameongeza kusema watu 10 wamejeruhiwa.

Kenya imeendelea kuchukua hatua kupunguza idadi za ajali ambazo zimekuwa zikiongezeka wakati ambapo watu wengi wa kapato cha kati wamekua wakinunua magari.

Jamaa za waathiriwa wakitizama magari yaliyoteketea Naivasha, Dec. 11, 2016.
Jamaa za waathiriwa wakitizama magari yaliyoteketea Naivasha, Dec. 11, 2016.

Mwaka 2013 serikali ilirudisha tena kipimo cha ulevi (breathlysers) ili kudhibiti ajali zinazonasibishwa na madreva walevi.

Kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Usafirishaji na Usalama takriban watu 1 574 wameuawa na ajali za barabarani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu ukilinganisha watu 86 waliuawa katika kipindi kama hiki mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG