Hatua hiyo ya serikali hata hivyo imeibua shutuma za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Mapigano yalizuka katika jimbo hilo mwezi Julai mwaka jana, kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa eneo hilo waitwao Fano, ambao wameishutumu serikali kwa kudhoofisha usalama wa eneo hilo.
Hali ya tahadhari iliipatia serikali mamlaka ya kuweka sheria za kutotoka nje, kuzuia harakati za watu na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu.
Tangu Agosti, vikosi vya serikali vimewaondoa wapiganaji wa Fano kutoka mijini, lakini mapigano yameendelea katika miji midogo na maeneo ya vijijini.
Bunge lilisema hatua ya kuongezewa kwa muda huo ilikubaliwa kufuatia ombi la waziri wa sheria, na mijadala kati ya wabunge.
Serikali inakanusha kuwa inalenga kudhoofisha usalama wa Amhara. Serikali haijajibu madai mahususi ya dhuluma huko Amhara lakini ilisema mwezi Novemba kwamba ripoti ya haki za binadamu nchini Ethiopia EHRC, kuhusu suala hilo haikuwa na ukweli.