Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:03

AU, Somalia na Ethiopia wakutana kuhusu mzozo wa bandari


Malori yakipokelewa misaada kwenye bandari ya Somaliland. Juli 21, 2018.
Malori yakipokelewa misaada kwenye bandari ya Somaliland. Juli 21, 2018.

Baraza la kusuluhisha mizozo la Umoja wa Afrika limekutana Jumatano wakati hali ya taharuki ikiongezeka kati ya Ethiopia na Somalia kuhusiana na mkataba wa ufukwe, wakati mataifa hayo yakiombwa kuwa tulivu.

Ethiopia isiyo na bandari ilitia saini mkataba wa usiotarajiwa na eneo la Somalia lililojitenga la Somaliland, Januari mosi, hatua ambayo Mogadishu imelalamikia ikidai kwamba ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Baraza la AU, la Amani na Usalama, limesema kwamba limesikiliza wawakilishi kutoka Ethiopia na Somalia, mjini Addis Ababa, wakati likiomba mataifa hayo jirani kuzingatia mazungumzo. Kupitia taarifa, baraza hilo limesema kwamba lina wasi wasi kutokana na taharuki inayoendelea, pamoja na uwezekano wake wa kuvuruga amani, usalama na udhabiti wa kieneo.

Chini ya mkataba iliyotiwa saini awali, Somaliland ilikubali kukodisha kilomita 20 za ufukwe wake kwa Ethiopia kwa muda wa miaka 50, ikiwa na lengo la kujenga kituo cha jeshi la wanamaji, pamoja na bandari ya kibiashara. Somaliland ilikuwa himaya ya Uingereza karibu na Ghuba ya Aden, na ilijitangazia uhuru wake kutoka Somalia 1991, ingawa haijatambuliwa kama taifa na jumuia ya kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG