Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:41

Marekani, AU waingilia kati kuutuliza mivutano huko Pembe ya Afrika


wanawake wa Somalia wamekusanyika kwa ajili ya maandamano yanayopinga makubaliano kati ya Ethiopia na Somaliland huko Mogadishu Januari 3,2024. Picha na Reuters
wanawake wa Somalia wamekusanyika kwa ajili ya maandamano yanayopinga makubaliano kati ya Ethiopia na Somaliland huko Mogadishu Januari 3,2024. Picha na Reuters

Umoja wa Afrika siku ya Alhamisi umeungana na Marekani kuutuliza mivutano ya kikanda kufuatia makubaliano yanayopingwa vikali kati ya Ethiopia na mkoa uliojitenga wa Somaliland.

Somalia iliapa kulilinda eneo lake baada ya makubaliano ya Jumatatu, ambayo iliyaelezea kuwa ni “uchokozi” na “shambulizi la wazi” kwa uhuru wake lililofanywa na jirani yake Ethiopia.

Waraka wa maelewano (MoU) inaipa Ethiopia isiyokuwa na bahari, nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, utashi wake wa muda mrefu kupata fursa ya kuifikia bahari ya Shamu kupitia Somaliland.

Mwenyekiti wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat, alitoa taarifa akitaka “utulivu na kuheshimiana ili kupunguza makali ya mvutano” kati ya Ethiopia na Somalia.

Amezitaka nchi hizo mbili kujihusisha na mchakato wa mashauriano “bila ya kuchelewa” ili kusuluhisha tofauti zao.

Siku ya Jumatano Marekani ilikataa kuitambua kimataifa Somaliland iliyojitenga na pia imetoa wito wa mazungumzo ili kuumaliza mgogoro huo.

Chanzo cha Habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG