Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:32

Somalia yasema kamanda mwandamizi wa al-Shabaab alilengwa katika shambulizi


Vikosi vya Usalama vikifanya doria nje ya jengo linashukiwa kushambuliwa na al- Shabaab. Picha na Hassan Ali ELMI / AFP.
Vikosi vya Usalama vikifanya doria nje ya jengo linashukiwa kushambuliwa na al- Shabaab. Picha na Hassan Ali ELMI / AFP.

Serikali ya Somalia imeripoti kuwa ikishirikiana na jeshi la Marekani imemlenga kamanda wa juu wa al- Shabaab kusini mwa nchi hiyo.

Waziri wa habari wa Somalia Daudi Aweis amesema katika chapisho kuwa operesheni hiyo “ililenga kumpunguzia nguvu kiongozi huyo anayehusika na kupanga mashambulizi ya kigaidi”

Serikali ya Somalia imesema shambulio hilo lilitokea katika mkoa wa Middle Juba hapo Decemba 17. Kamanda mwanamgambo huyo bado hajatambuliwa.

Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika, inayojulikana kama AFRICOM, imeithibitishia Sauti ya Amerika kuhusu usahihi wa ripoti ya serikali ya Somalia.

Mara ya mwisho shambulizi la anga la Marekani lililomlenga kamanda wa juu wa al Shabaab lilikuwa mwezi Mei ambapo katika shambulio hilo mkuu wa operesheni za nje za kundi la wanamgambo lenye itikadi kali Moallim Osman alijeruhiwa .

Osman alishutumiwa kwa kusimamia uandikishaji wa wapiganaji wa kigeni kulisaidia kundi la al Shabaab nchini Somalia katika mapigano yanayoendelea dhidi ya serikali ya Somalia.

Serikali ya Somalia imeapa kuliondoa kundi hiko. Lengo la wanamgambo ni kuanzisha serikali ambayo itakuwa katika misingi ya sheria ya kiislamu kwa tafsiri yao.

Forum

XS
SM
MD
LG