Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:03

Somalia yakataa kufanya mazunguzo kuhusu mzozo wa bandari na Somaliland


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Somalia imekataa kufanya aina yoyote ya mazungumzo na Ethiopia kuhusu mkataba wa Addis Ababa na eneo la Somalia lililojitenga la Somaliland, la kukodisha sehemu ya bandari yake, wakati viongozi taifa wa kieneo wakikutana Alhamisi ili kujadili mzozo huo wa kidiplomasia unaoendekea kutokota.

Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, makubaliano yaliotiwa saini Januari mosi yangepelekea Ethiopia kutambua uhuru wa Somaliland, wakati ikiruhusiwa kutumia sehemu ya bandari yake kwenye bahari ya Shamu, kwa njia ya kukodishwa.

Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia 1991, lakini kufikia sasa haijatambuliwa kama taifa na jumuia ya kimataifa. Mkataba wake na Ethiopia ambayo haina bandari umeghadhabisha Somalia, na kupelekea vita vya maneno, vikiwemo vitisho kutoka Somalia kwamba huenda ikaingia vitani kuzuia hatua hiyo kuendelea.

Hali hiyo imepelekea Umoja wa Afrika Jumatano kuomba pande zote kubaki tulivu.

Forum

XS
SM
MD
LG