Rais Abdel Fattah el-Sissi alikosoa makubaliano ya Ethiopia na eneo lililojitenga na kutoa wito kwa Ethiopia kutumia bandari za Somalia na Djibouti "kupitia nchi zingine," badala ya kujaribu kufanya kile alichokiita "kudhibiti eneo la nchi nyingine."
"Hatutaruhusu mtu yeyote kutishia Somalia au kuingilia ardhi yake," el-Sissi aliuambia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari mjini Cairo, akiandamana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.
“Hakuna mtu anayepaswa kujaribu kuwatisha ndugu wa Misri, hasa ikiwa ndugu zetu watatuomba tushirikiane nao,” alisema.
Somaliland, eneo ambalo liko kimkakati karibu na Ghuba ya Aden, lilijitenga na Somalia mwaka 1991 wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika mzozo ulioongozwa na wababe wa kivita. Eneo hilo limedumisha serikali yake licha ya kukosa kutambuliwa kimataifa.
Kiongozi wa Somaliland Muse Bihi Abdi alitia saini mkataba wa maelewano na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mapema mwezi huu ili kuruhusu Ethiopia kukodisha ukanda wa pwani wa kilomita 20 ili kuanzisha kituo cha jeshi la wanamaji.
Forum