Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:28

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azisihi  Addis Ababa na Mogadishu kufungua majadiliano


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa wanahabari wakati wa mkutano wa BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa wanahabari wakati wa mkutano wa BRICS mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumapili alizisihi  Addis Ababa na Mogadishu kufungua majadiliano  ili kusuluhisha mzozo wao kuhusu mkataba wa baharini wa Ethiopia na mkoa uliojitenga wa Somaliland.

Mivutano katika eneo la Pembe ya Afrika imeongezeka tangu Ethiopia isiyo na bahari ilipofikia makubaliano na Somaliland Januari mosi ambayo yanaipa njia inayotafutwa sana ya kuingia baharini.

Kwa upande wake, Somaliland ambayo ilijitangazia uhuru wake mwaka 1991 imesema Ethiopia itaipatia utambuzi rasmi. Addis Ababa haijathibitisha hili.

Somalia siku ya Alhamisi iliondoa upatanishi wowote na Ethiopia isipokuwa makubaliano hayo yafutwe na kuapa kuwa watapambana kwa njia zote za kisheria kuupinga.

Forum

XS
SM
MD
LG