Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:32

Zelenskyy: Vitendo vya uhalifu vya majeshi ya Russia vyafichuliwa na kuorodheshwa


Rais Volodymyr Zelenskyy akiwa na wapiganaji wa jeshi la Ukraine.
Rais Volodymyr Zelenskyy akiwa na wapiganaji wa jeshi la Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Ijumaa katika hotuba yake ya kila siku kuwa vitendo vya uhalifu vilivyofanywa na majeshi ya Russia katika mkoa wa Kharkiv wa Ukraine uliokombolewa vinafichuliwa na kuorodheshwa.

Zelenskyy alisema kuwa, hadi sasa, zaidi ya makaburi 440 yamefukuliwa katika eneo la maziko ya halaiki karibu na Izium” na ushahidi unajitokeza kuwa wanajeshi wa Russia “waliwapiga risasi waliozikwa kwa mashara.”

Miili iliyopatikana eneo lililofukuliwa na kukutwa kaburi la halaiki baada ya majeshi ya Ukraine kulikamata eneo la Izium, Ukraine, Sept. 16, 2022.
Miili iliyopatikana eneo lililofukuliwa na kukutwa kaburi la halaiki baada ya majeshi ya Ukraine kulikamata eneo la Izium, Ukraine, Sept. 16, 2022.

Zaidi ya hilo, alisema wanajeshi wa Russia wamewashikilia baadhi ya watu, wakiwemo wageni, mateka kwa miezi kadhaa. Ametaja raia saba wa Sri Lanka ambao walikuwa wanafunzi katika Chuo cha Udaktari cha Kupyansk Ukraine wakati wa uvamizi huo ambao wameshikiliwa mateka na Warussia tangu mwezi Machi.

“Ni hivi sasa tu, baada ya kuukomboa mkoa wa Kharkiv, watu hawa wameokolewa, wanapewa huduma sahihi ya afya,” alisema.

Zelenskyy pia alisema alizungumza siku ya Ijumaa na wawakilishi kutoka kampuni ya Nike. Alisema aliwashukuru “kwa uamuzi wao wa kuondoka kutoka soko la Russia. Ni uamuzi sahihi.

Huu ni mfano wa namna biashara inaweza kuchukua hatua muhimu katika kulinda ubinadamu na uhuru. Iwapo nchi imeamua kuchukua njia ya ugaidi, ni wajibu wa kila kampuni inayojiheshimu kukaa mbali na nchi kama hiyo.”

Wanajeshi wa Ukraine wakipumzika katika kijiji walichokikomboa hivi karibuni kaskazini ya Kharkiv, mashariki ya Ukraine, Mei 15, 2022
Wanajeshi wa Ukraine wakipumzika katika kijiji walichokikomboa hivi karibuni kaskazini ya Kharkiv, mashariki ya Ukraine, Mei 15, 2022

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumamosi kupitia ujumbe wa Twitter kuwa, “Ukraine inaendelea na operesheni za mashambulizi upande wa kaskazini mashariki wa nchi hiyo wakati majeshi ya Russia yameweka ngome ya ulinzi kati ya Mto Oskil na mji wa Svatove.

Russia huenda inachukulia kwamba kudhibiti ukanda huo ni muhimu kwa sababu ni kati ya njia muhimu inayopitisha mahitaji yanayopelekwa katika njia kadhaa ambazo Russia bado inazidhibiti kutoka mkoa wa Belgorod ya Russia.”

Na zaidi ya hilo, njia hii iko karibu na mpaka wa Luhansk Oblast, ambayo ni sehemu ya Donbas, ambayo Russia inakusudia ‘kuikomboa’ kama moja ya malengo yake ya vita ya hivi sasa,” wizara imesema. Imeongeza, “Kupoteza eneo kubwa la ardhi huko Luhansk utaharibu bila ya kificho Mkakati wa Russia.”

XS
SM
MD
LG