Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:13

Russia yatuma ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa Iran kushambulia Kyiv

Droni za Russia zashambulia Kyiv, Ukraine.
Droni za Russia zashambulia Kyiv, Ukraine.

Russia imeishambulia Ukraine usiku kucha kwa kile maafisa wa Ukraine walichosema Jumatatu ni wimbi la ndege zisizokuwa na rubani, zikilenga mashambulizi yake maeneo mbalimbali ikiwemo mji mkuu, Kyiv.

Russia imeishambulia Ukraine usiku kucha kwa kile maafisa wa Ukraine walichosema Jumatatu ni wimbi la ndege zisizokuwa na rubani, zikilenga mashambulizi yake maeneo mbalimbali ikiwemo mji mkuu, Kyiv.

Viongozi wa mji wamesema ulinzi wa anga wa Ukraine ulifanya kazi kwa kiasi kikubwa kuilinda Kyiv, ambapo baadhi ya uharibifu ulitokana na vipande vya droni zilizotunguliwa kuangukia katika majengo.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema Jumatatu kuwa Russia ilituma droni 40 kuushambulia mkoa wa Kyiv na kwamba zote hizo zilitunguliwa.

Russia imekuwa ikitumia droni zilizotengenezwa Iran maarufu kama Shahed kushambulia miji ya Ukraine na miundombinu.

Mashambulizi ya karibuni yalifuatia wimbi la shambulizi usiku kabla yake ambapo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema zilijumuisha Shahed 45 ambazo majeshi yake yalizitungua.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

“Vitendo vya kigaidi vya Russia vinasikitisha, na wameuanza mwaka huu na mwenendo ule ule,” Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya Jumapili .

Baadhi ya taarifa hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG