Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:43

Russia imepiga makombora 69 nchini Ukraine siku mbili kabla ya mwaka mpya


Watu wakijificha katika kituo cha treni chini ya ardhi kinachotumika kujikinga na mashambulizi ya mabomu ya Russia huko Kyiv, Ukraine, Dec. 29, 2022. (AP Photo/Efrem Lukatsky)
Watu wakijificha katika kituo cha treni chini ya ardhi kinachotumika kujikinga na mashambulizi ya mabomu ya Russia huko Kyiv, Ukraine, Dec. 29, 2022. (AP Photo/Efrem Lukatsky)

Wanajeshi wa Russia wamefyatua makombora kadhaa kuelekea Ukraine mapema Alhamisi, wakiulenga mji mkuu wa Kyiv, mji wa kaskazini mashariki wa Kharkiv na miji mingine.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limetungua makombora 54 kati ya 69 yaliyorushwa na Russia, katika shambulizi lililoanza saa moja asubuhi kwa saa za Ukraine.

Kamanda wa jeshi la Ukraine Brigadia General Oleksiy Hromov, amesema makombora hayo yamefyatuliwa kwenye mfumo muhimu na miundo mbinu ya nishati katika mikoa ya mashariki, katikati, magharibi na kusini mwa Ukraine.

Brigadia wa Oleksii Gromov: "Jeshi la Russia limetekeleza mashambulizi makubwa ndani ya eneo la Ukraine saa moja asubuhi. Makombora hayo yalikuwa ya kutoka angani na baharini na kutoka kwa ndege za kutekeleza mashambulizi.

Yalilenga mifumo muhimu ya nishati katika maeneo ya mashariki, katikati, magharibi na kusini mwa nchi. Adui ametumia zaidi ya makombora 69. Mfumo wetu wa ulinzi wa anga umeharibu makombora 54.

Shambulizi hilo lilifuatia shambulizi jingine lililotekelezwa usiku kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Russia imekuwa ikitekeleza mshambulizi ya makombora dhidi ya Ukraine katika miezi ya hivi karibuni, ikilenga mifumo ya nishati na kupelekea mamilioni ya watu kukosa umeme wakati huu wa kipindi cha baridi kali Ulaya.

Mashambulizi ya leo yametokea baada ya Russia kuukataa mpango wa amani wa Ukraine, ikisisitiza kwamba ni lazima Ukraine ikubali kuachilia mikoa minne ya Ukraine ambayo Russia imevamia na kuinyakua.

XS
SM
MD
LG