Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:22

Russia yazidisha mashambulizi ya makombora kwenye mji wa Ukraine wa Kherson


moshi mwingi waonekana baada ya mashambulizi ya Russia katika vitongoji vya mji wa Bakhmut, Ukraine, Disemba 27, 2022. Picha ya AP
moshi mwingi waonekana baada ya mashambulizi ya Russia katika vitongoji vya mji wa Bakhmut, Ukraine, Disemba 27, 2022. Picha ya AP

Vikosi vya Russia vimezidisha mashambulizi ya makombora na mizinga kwenye mji wa Kherson zaidi ya wiki sita baada ya mji huo kuchukuliwa tena na wanajeshi wa Ukraine na kuongeza shinikizo kwenye mstari wa mbele upande wa mashariki, jeshi la Ukraine limesema Jumatano.

Russia iliyashambulia zaidi ya makazi 25 karibu na Kherson na Zaporizhzhia, na kusababisha vifo vya raia na kuharibu miundombinu ya raia katika mji wa Kherson, mkuu wa jeshi la Ukraine amesema katika taarifa.

Reuters haikuweza kuhakikisha mara moja ripoti kuhusu mashambulizi hayo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amewahimiza wananchi wa Ukraine kuwakumbatia wapendwa wao, wawaambie marafiki kuwa wanawathamini, wawaunge mkono wafanyakazi wenzao, wawashukuru wazazi wao na wafurahi pamoja na watoto wao mara kwa mara.

XS
SM
MD
LG