Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:29

Uingereza yasema Russia inatarajiwa kuendeleza wimbi la mashambulizi ya masafa marefu kote Ukraine


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza katika kikao cha mawasilisho cha Kikosi cha Pamoja (JEF) mjini Riga, Latvia huku Volodomyr Zelensky akisikiliza Desemba 19, 2022. REUTERS
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza katika kikao cha mawasilisho cha Kikosi cha Pamoja (JEF) mjini Riga, Latvia huku Volodomyr Zelensky akisikiliza Desemba 19, 2022. REUTERS

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa mpya ya kijasusi uvamizi wa Russia  nchini Ukraine kwamba Russia inatarajiwa kuendeleza "wimbi kubwa" la mashambulizi ya masafa marefu kote Ukraine, hasa ikilenga mtandao wa usambazaji wa nishati.

Ripoti hiyo ya Jumamosi, iliyowekwa kwenye Twitter, ilisema, Russia kwa uhakika inatumia mbinu hii katika jaribio la kuzima ulinzi wa anga wa Ukraine. Hata hivyo, kuna uwezekano wa kweli kwamba Russia itabadili mtindo huu ili kushambulia tena katika siku zijazo katika jitihada za kudhoofisha ari ya wakazi wa Ukraine katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Viongozi hao wa Russia na Ukraine wanatazamiwa kutoa hotuba za Mwaka Mpya Jumamosi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na Rais wa Russia Vladimir Puttin wanatarajiwa kutoa tathmini zao kuhusu mapigano hayo na yanatarajiwa kudumu kwa muda gani.

Zelenskyy alisema Ijumaa kuwa Ukraine inaendelea kustahimili na kuzima mawimbi ya mashambulizi ya anga ya Russia na kwamba ulinzi wa anga wa Ukraine umefanywa imara zaidi kuliko hapo awali.

"Katika mwaka mpya," aliongeza, "ulinzi wa anga wa Ukraine utakuwa na nguvu zaidi, na ufanisi zaidi."

XS
SM
MD
LG