Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 23:19

Waziri Mkuu wa India awapongeza wafanyakazi waliookolewa, waliokwama kwa siku 17

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi (AP Photo/Rafiq Maqbool, File)
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi (AP Photo/Rafiq Maqbool, File)

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amezungumza kwa njia ya simu na wafanyakazi waliookolewa baada ya kufanikiwa kutolewa kutoka  kwenye njia ya chini kwa chini iliyobomoka baada ya kukwama kwa siku 17.

Gari la kubeba wagonjwa likiwa na wafanyakazi waliokolewa kutoka katika handaki la kupitisha magari linalojengwa lililobomoka huko Silkyara upande wa jimbo la India la kaskazini la Uttarakhand, Novemba 28, 2023. (Picha na AP).

Kuondolewa kwa wanaume 41 wafanyakazi wa kima cha chini kutoka kwenye baadhi ya majimbo masikini sana nchini India, kulianza zaidi ya saa sita baada ya waokoaji kuvunja katika vifusi kuelekea kwenye handaki hilo katika jimbo la Uttarakhand ambako walikwama tangu Novemba 12.

“ Tulikuwa 41 na wote kutoka majimbo tofauti, wote tulikuwa kama kaka , “ alisema hayo Saba Ahmed mmoja wa wafanyakazi 41 waliookolewa.

Wafanyakazi hao pia walimwambia Modi walikuwa wanatembea huko chini ya ardhi na kufanya mazoezi ya Yoga nyakati za asubuhi ambayo yaliwasaidia kuwa vizuri.

Wafanyakazi hao hivi sasa wako katika hospitali na wanatarajiwa kwenda kwenye majimbo yao baada ya madaktari kuwaruhusu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG