Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:32

Waziri ashitakiwa kwa Ufisadi Uganda


Mzee mmoja akiwa na watoto wake wamekaa nyumbani kwao huko Karamoja, Uganda, tarehe 24 Mei 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.
Mzee mmoja akiwa na watoto wake wamekaa nyumbani kwao huko Karamoja, Uganda, tarehe 24 Mei 2022. Picha na Badru KATUMBA/AFP.

Mahakama nchini Uganda siku ya Alhamisi imemfungulia mashtaka waziri wa serikali Mary Goretti Kitutu pamoja na kaka yake kwa kuilaghai serikali katika kesi ya nadra kwa mtumishi wa umma wa ngazi ya juu anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Waziri huyo na kaka yake walifikishwa mbele ya Mahakama ya Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kuiba mabati yaliyotengwa kwa ajili ya makazi ya eneo la watu maskini sana.

Ndugu hao walishtakiwa "kwa makosa mawili (ya) kuisababishia serikali hasara na kula njama ya kulaghai," Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Jane Frances Abodo, aliliambia shirika la habari la AFP.

Watuhumiwa wamewekwa rumande na watafikishwa tena mahakamani Aprili 12, alisema.

Mabati hayo yalitengwa kwa ajili ya makazi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu huko Karamoja, eneo ambalo halijaendelezwa na halina taratibu za kisheria lililoko kaskazini magharibi mwa Uganda kwenye mpaka wa Kenya na Sudan Kusini.

Kitutu ni waziri mwenye anayehusika na maendeleo ya Karamoja.

Kashfa hiyo ilisababisha shutuma kali kutoka kwa umma ingawaje ni katika nchi ambayo rushwa imekithiri katika serikali.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amesema mashtaka dhidi ya Kitutu ni "ni moshi unaozuia kuona" na kuituhumu serikali ya rais aliyekuwepo madarakani kwa muda mrefu Yoweri Museveni kuwa mbaya zaidi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG