Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:38

Mashoga Uganda watafuta pa kujificha


Wakimbizi wa LGBT kutoka Sudan Kusini, Uganda na DR Congo wakielekea kwenye maandamano wakidai kudai ulinzi katika ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lililoko Nairobi, Kenya, tarehe 17 Mei 2019. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Wakimbizi wa LGBT kutoka Sudan Kusini, Uganda na DR Congo wakielekea kwenye maandamano wakidai kudai ulinzi katika ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lililoko Nairobi, Kenya, tarehe 17 Mei 2019. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

"Watatukamata kwa sababu siwezi kujifanya siko hivyo," alisema Alex, ambaye ni shoga nchini Uganda, ambako wabunge wiki iliyopita walipitisha kile ambacho kimekosolewa kuwa miongoni mwa sheria kali sana duniani dhidi ya ushoga.

Sheria iliyopendekezwa inayojulikana kama mswaada wa Kupinga Ushoga mwaka 2023, ambao upo tayari kupelekwa kwa rais Yoweri Museveni, ambaye anakabiliwa na shinikizo kutoka Umoja wa Mataifa na Marekani kuukataa mswaada huo.

Mswada huo ulipitishwa katika kikao cha bunge huku ukiwa umefanyiwa marekebisho mengi, na si wabunge wala wachambuzi wanaoelewa vizuri kuhusu kitu gani sheria hiyo inaeleza.

Kama Museveni atausaini kuwa sheria, basi yeyote anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela wakati wale watarudiakufanya makosa hayo watahukumiwa kifo, kulingana na wanaharakati.

Wanaharakati wanabainisha kuwa Uganda iliacha kabisa kutoa adhabu ya kifo, na kuwa hukumu za kifo hubadilika moja kwa moja na kuwa vifungo vya maisha jela.

Lakini hii haitoi afuenii kwa raia wa Uganda ambao ni mashoga kama Alex mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limebadilishwa mara kadhaa kwasababu ya usalama wake.

Kutoka nchi jirani ya Kenya hadi Afrika Kusini hadi huko Ulaya na Amerika Kaskazini, Mashoga raia wa Uganda ambao tayari wanaishi uhamishoni, wanatoa vidokezo na ushauri kwa ajili ya ya kutafuta maeneo salama na mbinu za urasimu za uhamiaji.

Chanzo cha habari hi ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG